Makumbusho ya Mkwawa, Kalenga (km 15 magharibi ya Iringa) ⅼ Instagram: @mkwawa_museum / @mkwawa.heritage.museum


Kalenga ilikuwa makao makuu ya Chifu Mkwawa, ambaye alipingana na Wajerumani hadi mwaka 1898 alipojitoa uhai. Baada ya hapo, kichwa chake kilikatwa na kupelekwa Ujerumani. Kulingana na mkataba wa Versailles, kilirejeshwa mwaka 1954. Katika Makumbusho haya kuna fuvu la Chifu Mkwawa (linaloaminika kuwa lake), pamoja na silaha zake kama mikuki, ngao na bunduki. Nje ya jengo kuna makaburi ya Sapi Mkwawa, mrithi wake, na mjukuu wake Adam Sapi Mkwawa. Pia kuna mabaki ya ukuta wa ngome.
Taarifa zaidi kuhusu Chief Mkwawa
- Remembering the Dismembered (Erinnerung an koloniale Gewalt und die Rückführung von Vorfahren): Mtwa Mkwawa: www.rememberinghumanremains.wordpress.com/mkwawa/
- Who was Chief Mkwawa? The Legacy of Uhehe’s Resistance Leader: www.mkwawa.com