Makumbusho ya Maji Maji ilifunguliwa rasmi mwaka 1980, na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na ilijengwa na Mkuu wa Mkoa wa kipindi hicho aitwaye Dkt. Laurance Mtazama Gama akishirikiana na wananchi wa Mkoa wa Ruvuma ili kutambua mchango wa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kwa ushiriki wao katika kupigana vita vya Maji Maji.
Mnakaribishwa sana makumbusho ya vita vya maji maji ili muweze kujua historia ya vita vya maji maji, historia vya Wangoni pamoja na kujua tamaduni za watu wa mkoa wa Ruvuma. Kutembea Ukumbi wa maonesho na kupata historia ya vita vya Maji. Tembelea eneo la Makaburi walipowazika Mashujaa wa vita vya Majimaji wapatao 66, walionyongwa na Wajerumani tarehe 27, Februari 1906. Kila mwaka mwezi wa Februari kunakuwa na sherehe ya kitamaduni zinazowakumbuka. Tembelea Kaburi la Nduna Songea Luwafu Mbano aliyezikwa kiwiliwili bila kichwa na kichwa chake kipo Ujerumani mpaka sasa. Tembelea eneo walinyongewa Mashujaa wa vita vya Majimaji. Tembelea mahakama ya Mwanzo iliyotumiwa na Wajerumani kwa ajili ya kuwahukumu waafrika wote waliokuwa wanapinga utawala wao. Tembelea Peramiho eneo ambalo alikuwa anaishi Chifu wa Wangoni Mputa Gwazerapasi Gama na pia tembela Maposeni eneo ambalo wangoni walitumia kwa ajili ya kuabudia na baadae eneo hilo lilichomwa na Padri Fransiscus na baadae Padri huyo aliuliwa na askari wa Kingoni. Eneo alilouliwa Padri huyo wa Kijerumani umejengwa mnara wa kumbukumbu.
Makumbusho ya Maji Maji Mashujaa Street along Mahenge Road ⅼ, PO BOX 1249 Songea ⅼ Web: www.nmt.go.tz/historical-centers/majimaji-museum ⅼ E-Mail: majimaji@nmt.go.tz ⅼ Telefon: +255 0763707157 ⅼ Facebook & Instagram: Nationalmuseum Tanzania







