Decolonial Travel Guide Tanzania

KIGOMA

Kigoma ni mji wa bandari ulioko katika Ziwa Tanganyika, karibu na mipaka ya Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, magharibi mwa Tanzania. Mji huu ni kituo cha mwisho cha reli ya Central Line (zamani ikijulikana kama reli ya Tanganyika), njia ya reli inayopita katikati ya Tanzania kutoka pwani, kupitia mji mkuu Dodoma hadi magharibi. Kwa watalii wengi, Kigoma ni sehemu ya kuanzia kwa safari za kutembelea Hifadhi za Taifa za Gombe na Mahale, maarufu kwa makundi ya sokwe. Huko Ujiji kuna Makumbusho ya Livingstone Memorial ambayo hayajakosolewa sana. Makumbusho hayo yakikumbuka mkutano wa kihistoria kati ya mwandishi wa habari Henry Morton Stanley na mtafiti wa Afrika David Livingstone. Wote wawili walikuwa wakiwakilisha mawazo ya ukoloni na wanaonyeshwa kama “waokoaji weupe” (White Saviours). Jumba hili pia linaeleza kuhusu biashara ya utumwa Afrika ya Mashariki. Athari za usanifu wa majengo kutoka enzi za Afrika ya Mashariki ya Kijerumani bado zinaonekana Kigoma, zikiwemo Boma ya zamani, kanisa, shule na makaburi.