
Arusha, iliyoko kaskazini mashariki mwa Tanzania, ni jiji la kisasa lenye watu wa tamaduni mbalimbali, na linajulikana kama kitovu cha utalii. Kwa sababu ya ukaribu wake na Hifadhi maarufu za Taifa kama Serengeti na Ngorongoro, pamoja na idadi kubwa ya watalii, Arusha huitwa pia “Dar es Safari.” Ukoloni wa Wajerumani na Waingereza umeacha athari zake katika usanifu wa jiji pamoja na maeneo ya mashambani, ambapo mashamba ya kahawa na mkonge yalianzishwa. Wakati wa ukoloni, Arusha ilikuwa kituo muhimu cha biashara. Pia jiji hili lilikuwa na mchango mkubwa katika harakati za kupigania uhuru. Azimio la Arusha, ambamo Rais wa Kwanza wa Tanzania Julius Nyerere alieleza dhamira yake ya Ujamaa – mfumo wa ujamaa na kujitegemea – lilipata jina lake kutoka hapa Arusha.
Taarifa zaidi
- Podcast [Englisch]: Decolonial Memories: Thomas Fues with Dr Valence Silayo
- Exhibition Lindenmuseum Stuttgart: Celebrating Womanhood – Cultural heritage from Kilimanjaro

