
Azimio la Arusha lilielezea maono ya kisiasa ya Tanzania kuhusu mfumo wa Ujamaa, ambao kwa Kiswahili unamaanisha mshikamano wa kifamilia na kuishi kwa pamoja. Dhana ya kujitegemea kama msingi mkuu ilisisitiza uhuru na mapambano dhidi ya ukoloni wa mataifa ya Magharibi na Ulaya. Ili kuhifadhi kumbukumbu za harakati za uhuru na Ujamaa, makumbusho haya yaliwekwa katika jengo ambamo Azimio hilo liliamuliwa na chama tawala cha wakati huo, TANU. Makumbusho haya yanaelezea mabadiliko ya kijamii na kiuchumi ambayo yalichangia kuzaliwa kwa taifa la kisasa la Tanzania.
Arusha Declaration Museum ⅼ Makongoro Road near Uhuru Tower Round About ⅼ P.O BOX 7423 Arusha ⅼ Mobile +255 678 853477 ⅼ Email: adm@nmt.go.tz ⅼ Web: www.nmt.go.tz/pages/arusha-decleration-museum-2