Decolonial Travel Guide Tanzania

Arusha: National Natural History Museum

Natural History Museum in Arusha (c) Lena Mattmüller

Makumbusho haya yako katika Boma ya Kijerumani, iliyojengwa mwaka 1900 na Wajerumani. Hapa kuna maonyesho ya matokeo ya uchunguzi wa kihistoria na wa kisayansi kuhusu maisha ya kale, kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania – yakiwemo mabaki ya kale kutoka Bonde la Olduvai. Pia, kuna maonyesho ya wanyama na mimea wa Afrika Mashariki. Sehemu nyingine ya maonyesho inahusu historia ya utawala wa kikoloni wa Kijerumani kaskazini mwa Tanzania.

Taarifa zaidi

National Natural History Museum ⅼ Boma Road ⅼ P.O Box 2160 Arusha ⅼ Phone: +255 754 532193 ⅼ Email: naturalhistory@nmt.go.tz ⅼ Web: www.nmt.go.tz/pages/national-natural-history-museum