
Iringa Boma ni sehemu ya kujifunza, kushiriki na kupumzika, inayotoa fursa mbalimbali kushiriki urithi wa utamaduni wa Iringa. Ni mojawapo ya majengo ya zamani zaidi Iringa. Ilijengwa mwaka 1914 na Wajerumani kama hospitali ya kijeshi, kwa kutumia mtindo wa usanifu wa Kijerumani uliochanganya vipengele vya Kiafrika, Kiswahili na Ulaya. Baadaye Waingereza waliifanya kuwa kituo cha utawala hadi baada ya uhuru. Baada ya ukarabati mkubwa, ilifunguliwa tena 2016 kama makumbusho ya mkoa.
Mbali na maonesho yake, shirika Fahari Yetu linatoa ziara za kutembea mjini na kwenda Gangilonga Rock.
Iringa Boma – Makumbusho ya Mkoa na Kituo cha Utamaduni karibu na Clock Tower na Uhuru Park. S.L.P. 1308, Iringa. ⅼ Website: www.fahariyetu.net/activities/iringa-boma E-Mail: info@fahariyetu.net ⅼ Telefon: +255 26 2700032 ⅼ Facebook & Instagram: @iringa_boma