Decolonial Travel Guide Tanzania

KIGOMA: Meli Liemba

Liemba (c) Lena Mattmüller

Liemba ambayo imeegeshwa katika bandari ya Kigoma, inachukuliwa kuwa mojawapo ya meli za abiria za zamani kabisa duniani na ilikuwa ikifanya kazi hadi mwaka 2018. Kwa historia ya zaidi ya miaka 100, meli (Dampfer) hii ni alama ya uvumilivu na ustahimilivu katika Ziwa Tanganyika. Kwa mujibu wa taarifa za magazeti, kutokana na umuhimu wake wa kihistoria, meli hiyo inatarajiwa kukarabatiwa kufikia Julai 2026, ili iweze tena kutumika kwa usafirishaji wa abiria na mizigo. Meli hiyo ilijengwa nchini Ujerumani mwaka 1913 katika karakana ya meli ya Meyer, na mwanzoni iliitwa jina la gavana wa kikoloni Gustav Adolf Graf von Goetzen. Mwaka 1927, ilipewa jina jipya Liemba ambalo ni jina la Kiswahili kwa Ziwa Tanganyika. Meli hiyo ilisafirishwa kwa taabu kutoka Ujerumani ikiwa imefungwa katika zaidi ya makasha 5,000, kwa kutumia meli, reli, na wapagazi wa Afrika Mashariki hadi Ziwa Tanganyika ambako ilikusanywa na kukamilishwa. Wakati wa Vita ya Kwanza ya Dunia, Liemba ilitumika kama meli ya kivita. Vita hivyo vilipiganwa Afrika Mashariki dhidi ya majeshi ya Waingereza na Wabelgiji. Mwaka 1916, wakati majeshi ya Kijerumani yalipokuwa yakirudi nyuma, kamanda wao Paul von Lettow-Vorbeck alitoa amri meli hiyo izamishwe. Miaka kadhaa baadaye, meli hiyo ilitolewa ndani ya maji na — baada ya ukarabati mdogo — ikarudishwa tena katika huduma