Decolonial Travel Guide Tanzania

SONGEA

Zeichnung Songea Mbano

Rose Kangu

Baada ya ujio wa Wajerumani walianzisha utawala wao na kubadilisha utawala ambao mwafrika (mtanganyika) aliuzoea, sambama na hilo, Utawala wa kijerumani ulikuwa ni utawala wa mabavu na wakiunyonyaji usio jail utu wa mtu. Aidha wajerumani walipoanza kutawala Tanganyika walianzisha mambo yafuatayo: Wajerumani walianzisha mashamba  makubwa ya mazao ya biashara kama katani na pamba. Na walianzisha matumizi ya pesa na wakati huo mwafrika alizoea kubadilishana vitu kwa vitu. Pia wajerumani walianzisha kodi za aina mbalimbali ikiwepo kodi ya kichwa, kodi ya nyumba na kodi ya matiti. Waafrika walinyanganywa ardhi zao zenye rutuba,na kulazimishwa kulima mzao ya biashara. Pia waafrika walifanyishwa kazi ngumu na walilipwa mshahara mdogo sana.

Wangoni

Wangoni ni kabila lililotoka Afrika ya Kusini na huko Afrika ya Kusini walikimbia kutokana na mambo mbalimbali ambayo ni vita vya wenyewe kwa wenyewe, njaa kali na uhaba wa ardhi na hivyo wakakimbia nchi yao na kuanza kutafuta makazi katika maeneo mbalimbali lengo likiwa ni kupata maeneo ambayo wangeweka makazi yao ya kudumu, kwa ufupi wangoni wameweka makazi katika nchi nyingi zilizopo Afrika ikiwepo Tanzania, Zambia, Malawi na  nchi nyingine za Afrika. Wangoni ni kabila la watu wa Kusini mwa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Ruvuma, hasa katika eneo la Songea.

Nduna Songea Luafu Mbano

Nduna Songea Luafu Mbano ni kiongozi ambaye alikuwa msaidizi Mkuu wa Chifu Mputa Bin Gwazerapasi Gama, Chifu wa Kabila la wangoni, alikuwa ni mmojawapo kati ya manduna 12 wa Chifu Mputa Gama. Mji wa Songea unaitwa kwa jina lake. Alikuwa kiongozi hodari na shupavu sanaaa, (Amiri Jeshi) aliyekuwa anamiliki jeshi ya jadi, kiongozi huyu aliwasumbua sana Wajerumani kipindi cha vita vya maji maji, lakini baadae walimkamata. Kabla ya kumnyonga walitaka kumtumia kama kibaraka wao, yaani mtu atakayekuwa anatoa siri za waafrika wenzie, lakini Songea Mbano alikataa na hivyo Wajerumani wakamchukua na kumpeleka kunyongwa. Aidha alipokuwa ananyongwa Kamba yake ilikatika mara tatu na hivyo wakaamuru kumpiga risasi na kumuua. Baadae walimzika na baada ya siku kadhaaa walifukua kaburi lake na kukata kichwa chake na kukisafirisha kwenda Ujerumani na kipo huko mpaka leo.

Grab von Songea Mbano in Songea. Seiner Geschichte widmet sich der Film „Das leere Grab“ (c) Henriette Seydel

Vita vya Maji Maji

Kwa sababu ya jeuri, wizi wa ardhi, na sera za unyonyaji, wenyeji waliasi utawala wa kigeni. Katika maandamano, katika kiangazi cha 1905, Waafrika Mashariki waliharibu mashamba ya pamba ya Ujerumani na kubomoa, kupora, na kuchoma nyumba za Wajerumani. Wafanyakazi wa utawala walifukuzwa, na mitambo ya kijeshi ilishambuliwa. Maasi hayo yalikua vuguvugu kuu la upinzani. Vita vya Maji Maji vilianza mwaka wa 1905 hadi 1907. Watu wa dini, lugha, na tamaduni mbalimbali waliungana. Zaidi ya makabila ishirini kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Ruvuma, Pwani, Iringa, Mbeya, Lindi, Mtwara, Njombe, Iringa, Morogoro, na Songwe yalishiriki katika vita dhidi ya utawala wa kigeni.

Mikoa yote iliunganishwa na dawa ya maji maji ilitengenezwa  na Mganga wa kienyeji aitwaye Kinjekitile Ngwale, dawa ya Majimaji ilitengenezwa mwaka 1904 na kuanza kusambazwa mwaka huohuo 1904. Dawa ya maji maji ilikuwa na masharti mbalimbali ili iweze kufanya kazi kwa ufanisi, baadhi ya  masharti hayo ni: Kutokula ugali wa muhogo, Kutokulala na mwanamke unapotumia dawa, Unapigana vita macho mbele kumfosi adui. Hapo awali, walikuwa bora zaidi na wakihamasishwa na matarajio ya maji, wapiganaji walipata mafanikio ya haraka. Waliweka karibu nusu ya eneo la kikoloni chini ya udhibiti wao.

Wajerumani walipigwa na mshangao na mwanzoni walikosa rasilimali za kutosha za kijeshi. Hata hivyo, kutokana na silaha za kisasa zaidi na kuongezeka kwa Ujerumani Schutztruppe, wapiganaji wa upinzani walizidi kuwa na aibu. Kwa hiyo walibadili mbinu za msituni na mashambulizi ya kushtukiza.

Wajerumani walijibu kwa sera ya ardhi iliyoungua. Waliharibu na kuangamiza visima, mashamba, mazao, mifugo na nyumba kusini mwa Tanzania. Watu walinyimwa riziki zao na kufa njaa. Wanahistoria wanakadiria kwamba jumla ya watu kati ya 180,000 na 300,000 waliuawa.

Taarifa zaidi
  • Becker, Felicitas & Beez, Jigal (2005): Der Maji-Maji-Krieg in Deutsch-Ostafrika 1905-1907. Berlin: Ch. Links Verlag.
  • Ebner, Fr Elzear (1987): The History of Wangoni, Peramiho: Benedictine Publications Ndanda
  • Film: Das Leere Grab / Kaburi la Wazi / Empty Grave (Deutschland/Tansania 2024)
  • Giblin, James und Monson, Jamie (2010): Maji Maji – Lifting the Fog of War, Leiden: Brill
  • Gwassa, Gilbert Clement Kamana, (1973/2005): The Outbreak and Development of the Maji Maji War 1905–1907, Köln: Rüdiger Koppe Verlag
  • LeGall, Yann & Mboro, Mnyaka Sururu (2021): Remembering the Dismembered. African Human Remains and Memory Cultures in and after Repatriation: Songea Mbanowww.rememberinghumanremains.wordpress.com/songea-mbano/
  • Riel, Art van (2023):  Der verschwiegene Völkermord. Deutsche Kolonialverbrechen in Ostafrika, Köln: Papy Rossa Verlag