Decolonial Travel Guide Tanzania

IRINGA

Jimson Sanga

Kwa kutumia Mwongozo huu wa safari wenye mtazamo wa kujikwamua na ukoloni (dekolonia) (Decolonial Travel Guide) kuhusu Iringa, ninataka kuonesha maeneo ya kihistoria ya Tanzania, nikisisitiza upinzani wa watu wake dhidi ya utawala wa kikoloni. Makala hii inaangazia maeneo muhimu yanayoakisi harakati za ukombozi, hasa ushujaa wa Wahehe chini ya uongozi wa Chifu Mkwawa. Kuanzia kujitoa mhanga kwa Sengimba huko Kikongoma, hadi Mapambano ya Lugalo na mauaji ya kikatili ya Kitanzini, kila eneo linabeba simulizi lenye nguvu kuhusu ushujaa, uasi, na kumbukumbu ya historia ya ukoloni wa Tanzania.

Kikongoma: Daraja la Mungu – Eneo la Kihistoria la Kuheshimu Ushujaa wa Mwanamke wa Kihehe

Wakati wa utawala wa Chifu Munyigumba, baba yake Chifu Mkwawa, alikuwepo shujaa mwenye nguvu aitwaye Mwambambe ambaye alilewa katika milki ya Chifu Munyigumba. Hata hivyo, Mwambambe hakuwa mzaliwa wa ukoo wa Khehe, jambo lililomfanya akose kukubalika kikamilifu kama kiongozi. Baada ya kifo cha Munyigumba, Mwambambe alijaribu kuchukua utawala kwa nguvu. Katika wakati huo, mtu pekee aliyekuwa na mamlaka ya kufanikisha ibada ya kumtawaza Chifu mpya wa Kihehe alikuwa Sengimba, mama yake Mkwawa. Mwambambe alimlazimisha Sengimba ampe dawa ya kiapo ili kuhalalisha utawala wake. Sengimba alimwambia kwamba dawa hiyo ya siri ilipatikana tu Kikongoma, eneo lenye miamba iliyopangwa vizuri na kijito kidogo cha Mto Ruaha kikipita chini yake. Mwambambe alimruhusu Sengimba aende peke yake kuchukua dawa. Lakini alipofika Kikongoma, Sengimba alitupa mwili wake kwenye ufa wenye maji mwingi ndani ya mawe, akijitoa mhanga kwa hiari badala ya kuisaliti nchi yake kwa mgeni.

Kikongoma God’s Bridge (c) Herry Titus Sanga – Fahari Yetu

Kikongoma leo hii ni alama ya ushujaa wa wanawake wa Khehe na ujasiri wa kupinga ukoloni. Ni eneo la kumbukumbu, motisha, na mshikamano wa mapambano ya ukombozi.

Uwanja wa Vita wa Lugalo: Alama Kuu ya Mapambano dhidi ya Ukoloni Tanzania

Uwanja wa vita wa Lugalo ni mahali ambapo Wahehe, wakiongozwa na Chifu Mkwawa, walipambana vikali dhidi ya Wajerumani mwishoni mwa mwaka 1891. Wanajeshi wa Ujerumani, chini ya Emil von Zelewsky, walivamia milki ya Khehe wakiwa zaidi ya askari 300. Licha ya kuwa na silaha duni, jeshi la Mkwawa lilitumia mbinu za kivita za hali ya juu walizojifunza kwa Wangoni na kuwashinda Wajerumani. Ushindi huu ulimfanya Mkwawa kujulikana kimataifa na kuonesha kuwa Himaya ya Khehe ilikuwa moja ya ngome madhubuti za kupinga ukoloni barani Afrika. Leo, eneo hili ni alama ya historia ya ukombozi wa Tanzania, likikumbusha ujasiri wa Chifu Mkwawa na watu wake. Wajerumani hata walijenga mnara wa kumbukumbu kwenye eneo hilo mapema miaka ya 1900.

Monument in Lugalo for German Soldiers (c) Jimson Sanga

Kitanzini: Sehemu ya Kumbukumbu ya Unyama wa Ukoloni wa Kijerumani dhidi ya Wahehe

Kitanzini ni eneo la kihistoria mjini Iringa linalokumbusha mauaji ya hadharani yaliyofanywa na wakoloni wa Kijerumani dhidi ya Wahhehe. Jina linatokana na “kitanzi” – kwa maana ya kamba ya kunyonga. Eneo hili lilitumika kunyonga hadharani wapiganaji, viongozi wa kisiasa, na raia wa kawaida waliotuhumiwa kuunga mkono harakati za upinzani wa Chifu Mkwawa. Kati ya waliouawa ni Mpangile Wangimbo, mdogo wa Chifu Mkwawa, aliyekataa kushirikiana na Wajerumani. Alinyongwa mwaka 1896 kwa kuasi, lakini kifo chake hakikuwazuia Wahhehe kuendelea kupigania uhuru wao.

Leo, Kitanzini ni eneo la majonzi lakini pia la kumbukumbu na msimamo wa kupinga utawala wa kigeni.

Kalenga: Ngome Kuu ya Kihistoria ya Iringa Wakati wa Ukoloni wa Kijerumani

Kalenga ni moja ya maeneo muhimu sana kihistoria katika mkoa wa Iringa. Baada ya ushindi wa vita vya Lugalo, Chifu Mkwawa alijenga ngome kubwa Kalenga kuilinda milki yake. Ngome hiyo ilijengwa kwa ustadi mkubwa na kulindwa na wapiganaji hodari. Hata hivyo, mwaka 1894, Wajerumani walishambulia Kalenga kwa kutumia mizinga na silaha nzito. Mkwawa alifanikiwa kutoroka na kujificha Mlambalasi. Leo Kalenga ni alama ya mapambano ya ukombozi, kitovu cha mipango ya vita na utawala wa Kihehe.

Kalenga Fort Map in 1896 (c) Fahari Yetu

Trotz des verheerenden Angriffs gelang es Chief Mkwawa dank seines Mutes und seiner Widerstandsfähigkeit zu fliehen und in Mlambalasi Zuflucht zu suchen. Bis heute ist Kalenga ein Symbol der afrikanischen Befreiung, insbesondere für die Wahehe. Es war nicht nur eine militärische Festung, sondern auch ein Zentrum für strategische Kriegsplanung, Regierungsführung und den Kampf gegen die deutsche Kolonialherrschaft.

Mlambalasi: Mapumziko ya Mwisho ya Chifu Mkwawa

Mlambalasini eneo la kihistoria linalohusishwa na mwisho wa maisha ya Chifu Mkwawa. Baada ya kushindwa Kalenga, Mkwawa alijificha katika mapango ya Mlambalasi na kuendesha vita vya msituni kwa miaka minne. Mwaka 1898, Wajerumani walipomgundua, Mkwawa alikataa kukamatwa na badala yake alijitoa uhai kwa kutumia bunduki yake. Alizikwa Mlambalasi, huku fuvu lake likichukuliwa Ujerumani. Baadaye lilirejeshwa na sasa lipo Makumbusho ya Mkwawa Kalenga. Mlambalasi leo ni ishara ya ushujaa na kujitoa kwa ajili ya kupinga ukoloni.

Chief Mkwawa Grave at Mlambalasi (c) Fahari Yetu